Zab. 92:5-8 Swahili Union Version (SUV)

5. Ee BWANA, jinsi yalivyo makuu matendo yako!Mawazo yako ni mafumbo makubwa.

6. Mtu mjinga hayatambui hayo,Wala mpumbavu hayafahamu.

7. Wasio haki wakichipuka kama majaniNa wote watendao maovu wakistawi.Ni kwa kusudi waangamizwe milele;

8. Bali Wewe, BWANA, U Mtukufu hata milele.

Zab. 92