Zab. 85:4-8 Swahili Union Version (SUV)

4. Mungu wa wokovu wetu, uturudishe,Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.

5. Je! Utatufanyia hasira hata milele?Utadumisha ghadhabu kizazi hata kizazi?

6. Je! Hutaki kurudi na kutuhuisha,Watu wako wakufurahie?

7. Ee BWANA, utuonyeshe rehema zako,Utupe wokovu wako.

8. Na nisikie atakavyosema Mungu BWANA,Maana atawaambia watu wake amani,Naam, na watauwa wake pia,Bali wasiurudie upumbavu tena.

Zab. 85