10. Hawakulishika agano la Mungu;Wakakataa kuenenda katika sheria yake;
11. Wakayasahau matendo yake,Na mambo yake ya ajabu aliyowaonyesha.
12. Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu,Katika nchi ya Misri, konde la Soani.
13. Aliipasua bahari akawavusha;Aliyasimamisha maji mfano wa chungu.
14. Akawaongoza kwa wingu mchana,Na usiku kucha kwa nuru ya moto.
15. Akapasua miamba jangwani;Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi.
16. Akatokeza na vijito gengeni,Akatelemsha maji kama mito.
17. Lakini wakazidi kumtenda dhambi,Walipomwasi Aliye juu katika nchi ya kiu.