Zab. 73:21-24 Swahili Union Version (SUV)

21. Moyo wangu ulipoona uchungu,Viuno vyangu viliponichoma,

22. Nalikuwa kama mjinga, sijui neno;Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako.

23. Walakini mimi ni pamoja nawe daima,Umenishika mkono wa kuume.

24. Utaniongoza kwa shauri lako,Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.

Zab. 73