5. Basi adui na anifuatie,Na kuikamata nafsi yangu;Naam, aukanyage uzima wangu,Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
6. BWANA uondoke kwa hasira yako;Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu;Uamke kwa ajili yangu;Umeamuru hukumu.
7. Kusanyiko la mataifa na likuzunguke,Na juu yake uketi utawale.