Zab. 68:25-31 Swahili Union Version (SUV)

25. Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda,Kati ya wanawali wapiga matari.

26. Mhimidini Mungu katika mikutano,Bwana katika makusanyiko ya Israeli.

27. Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao;Wakuu wa Yuda, kundi lao;Wakuu wa Zabuloni;Wakuu wa Naftali.

28. Ee Mungu, uziamuru nguvu zako;Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu.

29. Kwa ajili ya hekalu lako YerusalemuWafalme watakuletea hedaya.

30. Mkemee mnyama wa manyasini;Kundi la mafahali, na ndama za watu;Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha,Uwatawanye watu wapendao vita.

31. Masheki watakuja kutoka Misri,Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara.

Zab. 68