Zab. 65:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.

9. Umeijilia nchi na kuisitawisha,Umeitajirisha sana;Mto wa Mungu umejaa maji;Wawaruzuku watu nafakaMaana ndiwe uitengenezaye ardhi.

10. Matuta yake wayajaza maji;Wapasawazisha palipoinuka,Wailainisha nchi kwa manyunyu;Waibariki mimea yake.

11. Umeuvika mwaka taji ya wema wako;Mapito yako yadondoza unono.

12. Huyadondokea malisho ya nyikani,Na vilima vyajifunga furaha.

Zab. 65