Zab. 44:19-23 Swahili Union Version (SUV)

19. Hata utuponde katika kao la mbwa-mwitu,Na kutufunika kwa uvuli wa mauti.

20. Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu,Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu;

21. Je! Mungu hatalichunguza neno hilo?Maana ndiye azijuaye siri za moyo.

22. Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;Tunafanywa kondoo waendao kuchinjwa.

23. Amka, Bwana, mbona umelala?Ondoka, usitutupe kabisa.

Zab. 44