17. Haya yote yametupata, bali hatukukusahau,Wala hatukulihalifu agano lako.
18. Hatukuiacha mioyo yetu irudi nyuma,Wala hatua zetu hazikuiacha njia yako.
19. Hata utuponde katika kao la mbwa-mwitu,Na kutufunika kwa uvuli wa mauti.
20. Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu,Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu;
21. Je! Mungu hatalichunguza neno hilo?Maana ndiye azijuaye siri za moyo.
22. Hasha! Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;Tunafanywa kondoo waendao kuchinjwa.
23. Amka, Bwana, mbona umelala?Ondoka, usitutupe kabisa.
24. Mbona unatuficha uso wako,Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu?