4. Nami nalisema, BWANA, unifadhili,Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.
5. Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,Atakufa lini, jina lake likapotea?
6. Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,Moyo wake hujikusanyia maovu,Naye atokapo nje huyanena.
7. Wote wanaonichukia wananinong’ona,Wananiwazia mabaya.
8. Neno la kisirani limemgandama,Na iwapo amelala hatasimama tena.
9. Msiri wangu tena niliyemtumaini,Aliyekula chakula changu,Ameniinulia kisigino chake.
10. Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,Uniinue nipate kuwalipa.