5. Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,Na neno lake nimelitumainia.
6. Nafsi yangu inamngoja Bwana,Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,Naam, walinzi waingojao asubuhi.
7. Ee Israeli, umtarajie BWANA;Maana kwa BWANA kuna fadhili,Na kwake kuna ukombozi mwingi.