3. Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;Uyatie nuru macho yangu,Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4. Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5. Nami nimezitumainia fadhili zako;Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.