Zab. 119:94-100 Swahili Union Version (SUV)

94. Mimi ni wako, uniokoe,Kwa maana nimejifunza mausia yako.

95. Wasio haki wameniotea ili kunipoteza,Nitazitafakari shuhuda zako.

96. Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho,Bali agizo lako ni pana mno.

97. Sheria yako naipenda mno ajabu,Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.

98. Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu,Kwa maana ninayo sikuzote.

99. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.

100. Ninao ufahamu kuliko wazee,Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.

Zab. 119