Zab. 116:3-8 Swahili Union Version (SUV)

3. Kamba za mauti zilinizunguka,Shida za kuzimu zilinipata.Naliona taabu na huzuni;

4. Nikaliitia jina la BWANA.Ee BWANA, nakuomba sana,Uniokoe nafsi yangu.

5. BWANA ni mwenye neema na haki,Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.

6. BWANA huwalinda wasio na hila;Nalidhilika, akaniokoa.

7. Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako,Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.

8. Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,Macho yangu na machozi,Na miguu yangu na kuanguka.

Zab. 116