2. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3. Naye atakuwa kama mti uliopandwaKandokando ya vijito vya maji,Uzaao matunda yake kwa majira yake,Wala jani lake halinyauki;Na kila alitendalo litafanikiwa.
4. Sivyo walivyo wasio haki;Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5. Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.