21. Basi miji ya kabila ya wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni Yeriko, na Beth-hogla, na Emek-kesisi,
22. na Bethiaraba, na Semaraimu, na Betheli;
23. na Avimu, na Para, na Ofra;
24. na Kefar-amoni, na Ofni, na Geba; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake;
25. na Gibeoni, na Rama, na Beerothi;
26. na Mispa, na Kefira, na Moza;
27. na Rekemu, na Irpeeli, na Tarala;
28. na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kuandama jamaa zao.