Yos. 13:14-21 Swahili Union Version (SUV)

14. Lakini hakuwapa watu wa kabila ya Lawi urithi uwao wote; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.

15. Musa akawapa kabila ya wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao.

16. Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba;

17. na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni;

18. na Yahasa, na Kedemothi, na Mefaathi;

19. na Kiriathaimu, na Sibma, na Sereth-shahari katika kilima cha hilo bonde;

20. na Beth-peori, na nchi za matelemko ya Pisga, na Beth-yeshimothi;

21. na miji yote ya nchi tambarare, na ufalme wote wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akitawala katika Heshboni, aliyepigwa na Musa pamoja na hao wakubwa wa Midiani, nao ni Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao mashehe wa Sihoni, waliokuwa katika nchi hiyo.

Yos. 13