41. Yoshua akawapiga kutoka Kadesh-barnea mpaka Gaza, na nchi yote ya Gosheni, hata Gibeoni.
42. Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akatwaa, wakati huo, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli,
43. Kisha Yoshua akarudi, na Israeli wote pamoja naye, hata marago yao huko Gilgali.