Yoe. 1:9-13 Swahili Union Version (SUV)

9. Sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.

10. Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.

11. Tahayarini, enyi wakulima;Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;Kwa ajili ya ngano na shayiri,Maana mavuno ya mashamba yamepotea.

12. Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;Naam, miti yote ya mashamba imekauka;Maana furaha imekauka katika wanadamu.

13. Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani;Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;Njoni mlale usiku kucha katika magunia,Enyi wahudumu wa Mungu wangu;Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.

Yoe. 1