5. Levukeni, enyi walevi, mkalie;Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai;Kwa sababu ya divai mpya;Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
6. Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu,Lenye nguvu, tena halina hesabu;Meno yake ni kama meno ya simba,Naye ana magego ya simba mkubwa.
7. Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
8. Ombolea kama mwanamwali avaaye maguniaKwa ajili ya mume wa ujana wake.