17. Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.
18. Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi;
19. na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.
20. Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.
21. Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.