Yer. 8:20-22 Swahili Union Version (SUV)

20. Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.

21. Kwa sababu ya maumivu ya binti ya watu wangu nimeumia mimi; nimevaa kaniki; ushangao umenishika.

22. Je! Hapana zeri katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?

Yer. 8