12. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
13. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
14. Nami nitaonekana kwenu, asema BWANA, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema BWANA; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka.
15. Maana mmesema, BWANA ametuinulia manabii huko Babeli.
16. Maana BWANA asema hivi, katika habari za mfalme aketiye katika kiti cha enzi cha Daudi, na katika habari za watu wote wakaao ndani ya mji huu, ndugu zenu wasiokwenda pamoja nanyi kufungwa;