Wim. 5:4-8 Swahili Union Version (SUV)

4. Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni,Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.

5. Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu;Mikono yangu ilidondoza manemane,Na vidole vyangu matone ya manemane,Penye vipini vya komeo.

6. Nalimfungulia mpendwa wangu,Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita;(Nimezimia nafsi yangu aliponena),Nikamtafuta, nisimpate,Nikamwita, asiniitikie.

7. Walinzi wazungukao mjini waliniona,Wakanipiga na kunitia jeraha,Walinzi walindao kuta zakeWakaninyang’anya shela yangu.

8. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Ninyi mkimwona mpendwa wangu,Ni nini mtakayomwambia?Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.

Wim. 5