2. Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho,Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha!Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu,Hua wangu, mkamilifu wangu,Kwa maana kichwa changu kimelowa umande,Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
3. Nimeivua kanzu yangu; niivaeje?Nimeitawadha miguu; niichafueje?
4. Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni,Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.
5. Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu;Mikono yangu ilidondoza manemane,Na vidole vyangu matone ya manemane,Penye vipini vya komeo.