Wim. 3:7-10 Swahili Union Version (SUV)

7. Tazama, ni machela yake Sulemani;Mashujaa sitini waizunguka,Wa mashujaa wa Israeli.

8. Wote wameshika upanga,Wamehitimu kupigana;Kila mtu anao upanga wake pajaniKwa hofu ya kamsa za usiku.

9. Mfalme Sulemani alijifanyizia machelaYa miti ya Lebanoni;

10. Nguzo zake alizifanyiza za fedha,Na mgongo wake wa dhahabu,Kiti chake kimepambwa urujuani,Gari lake limenakishiwa njumu,Hiba ya binti za Yerusalemu.

Wim. 3