Rum. 15:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;

9. tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa,Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa,Nami nitaliimbia jina lako.

10. Na tena anena,Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake.

11. Na tena,Enyi Mataifa yote, msifuni Bwana;Enyi watu wote, mhimidini.

12. Na tena Isaya anena,Litakuwako shina la Yese,Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

Rum. 15