Rum. 12:8-15 Swahili Union Version (SUV)

8. mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.

9. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.

10. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

11. kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;

12. kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;

13. kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

14. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

15. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

Rum. 12