Oba. 1:3-6 Swahili Union Version (SUV)

3. Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,Wewe ukaaye katika pango za majabali,Mwenye makao yako juu sana;Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?

4. Ujapopanda juu kama tai,Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota,Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.

5. Kama wevi wangekujilia, kama wanyang’anyi wangekujilia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujilia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe?

6. Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwa-tafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwa-ulizwa!

Oba. 1