60. Wanethini wote, pamoja na akina watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
61. Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;
62. Wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita na arobaini na wawili.
63. Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.