55. wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema;
56. wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
57. Akina watumwa wa Sulemani; Wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda;
58. wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli;
59. wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni.
60. Wanethini wote, pamoja na akina watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
61. Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;