4. Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.
5. Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
6. Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya;
7. akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.
8. Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;