Mwa. 46:7-14 Swahili Union Version (SUV)

7. Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.

8. Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli walioingia Misri, Yakobo na wanawe: Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.

9. Na wana wa Reubeni; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.

10. Na wana wa Simeoni; Yemueli na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli, mwana wa mwanamke Mkanaani.

11. Na wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.

12. Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.

13. Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni.

14. Na wana wa Zabuloni; Seredi, na Eloni, na Yaleeli.

Mwa. 46