Mwa. 35:24-27 Swahili Union Version (SUV)

24. Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini.

25. Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali.

26. Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.

27. Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Ibrahimu na Isaka.

Mwa. 35