13. Ikawa hapo Mungu aliponisafirisha kutoka nyumba ya baba yangu, nikamwambia, Hii ndiyo fadhili yako, utakayonifanyia. Kila mahali tuingiapo, useme, Huyu ni ndugu yangu.
14. Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Ibrahimu, akamrudishia Sara mkewe.
15. Abimeleki akasema, Nchi yangu iko mbele yako, kaa upendapo.
16. Naye akamwambia Sara, Tazama! Nimempa ndugu yako fedha elfu, itakuwa kifunika macho kwako mbele ya wote walio pamoja nawe, nawe utakuwa na haki mbele ya watu wote.
17. Ibrahimu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.