Mt. 5:40-42 Swahili Union Version (SUV)

40. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.

41. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.

42. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Mt. 5