4. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
5. Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6. Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda;Kwa kuwa kwako atatoka mtawalaAtakayewachunga watu wangu Israeli.