13. Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
14. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema,Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa;Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
15. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito,Na kwa masikio yao hawasikii vema,Na macho yao wameyafumba;Wasije wakaona kwa macho yao,Wakasikia kwa masikio yao,Wakaelewa kwa mioyo yao,Wakaongoka, nikawaponya.
16. Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.
17. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
18. Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.