Mt. 13:12-17 Swahili Union Version (SUV)

12. Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

13. Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.

14. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema,Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa;Kutazama mtatazama, wala hamtaona.

15. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito,Na kwa masikio yao hawasikii vema,Na macho yao wameyafumba;Wasije wakaona kwa macho yao,Wakasikia kwa masikio yao,Wakaelewa kwa mioyo yao,Wakaongoka, nikawaponya.

16. Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.

17. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.

Mt. 13