13. Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili.
14. Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.
15. Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
16. akawakataza wasimdhihirishe;
17. ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
18. Tazama, mtumishi wangu niliyemteua;Mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye;Nitatia roho yangu juu yake,Naye atawatangazia Mataifa hukumu.