5. Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.
6. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
7. Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
9. Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;
10. wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake.