14. Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;
15. Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;
16. Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
17. Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.