Mk. 4:39-41 Swahili Union Version (SUV)

39. Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

40. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

41. Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Mk. 4