Mk. 4:2-4 Swahili Union Version (SUV)

2. Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake,

3. Sikilizeni; Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda;

4. ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila.

Mk. 4