Mit. 6:3-7 Swahili Union Version (SUV)

3. Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe,Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako;Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako.

4. Usiache macho yako kupata usingizi,Wala kope za macho yako kusinzia.

5. Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji,Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.

6. Ewe mvivu, mwendee chungu,Zitafakari njia zake ukapate hekima.

7. Kwa maana yeye hana akida,Wala msimamizi, wala mkuu,

Mit. 6