Mit. 6:15-21 Swahili Union Version (SUV)

15. Basi msiba utampata kwa ghafula;Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona.

16. Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA;Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

17. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo,Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

18. Moyo uwazao mawazo mabaya;Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;

19. Shahidi wa uongo asemaye uongo;Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

20. Mwanangu, shika maagizo ya baba yako,Wala usiiache sheria ya mama yako.

21. Yafunge hayo katika moyo wako daima;Jivike hayo shingoni mwako.

Mit. 6