16. Huangalia shamba, akalinunua;Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;Hutia mikono yake nguvu.
18. Huona kama bidhaa yake ina faida;Taa yake haizimiki usiku.
19. Hutia mikono yake katika kusokota;Na mikono yake huishika pia.
20. Huwakunjulia maskini mikono yake;Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.