12. Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe?Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
13. Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani,Simba yuko katika njia kuu.
14. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake;Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.
15. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake.
16. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake,Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.
17. Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake;Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.
18. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge,Na mishale, na mauti;
19. Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake,Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?
20. Moto hufa kwa kukosa kuni;Na bila mchongezi fitina hukoma.
21. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka,Na kama kuni juu ya moto;Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.
22. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo.Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.