Mit. 21:1-2 Swahili Union Version (SUV)

1. Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA;Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo.

2. Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huipima mioyo.

Mit. 21