8. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,Wala usiiache sheria ya mama yako,
9. Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako,Na mikufu shingoni mwako.
10. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi,Wewe usikubali.
11. Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi,Na tuvizie ili kumwaga damu;Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;
12. Tuwameze hai kama kuzimu,Na wazima, kama wao washukao shimoni.